Saturday, 13 January 2018

MAGUFULI AZUNGUMZA KUHUSU KUONGEZA MIAKA YA MADARAKA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli ameweka wazi kuwa hana mpango wowote wa kuongeza muda wa kukaa madarakani kutoka miaka 5-7 na pia hafurahishwi na mijadala hiyo. 



Rais Magufuli ameyasema hayo leo Januari 13 wakati alipokutana na Katibu wa Itikadi na Uenezi  IKulu, ndg. Humphrey Polepole na kumtuma awajulishe watanzania na wana CCM kwamba wapuuze mijadala hiyo kwani jambo hilo halijawahi kujadiliwa katika kikao chochote cha chama.

Kupitia taarifa iliyotlewa na Ikulu, Rais Magufuli amemuagiza Polepole kuwajulisha watanzania na wana CCM kuwa wasikubali kuyumbishwa au kupotoshwa na mambo yasiyokuwa ya msingi na badala yake wajielekeze katika kukuza uchumi na kutekeleza ilani ya CCM ya mwaka 2017.

No comments:

Watumiaji wa Barabara Watakiwa Kutii Sheria za Usalama

Mkuu wa Kitengo cha Usalama barabarani Mkoa wa Kilimanjaro Mrakibu Msaidizi wa Polisi Sauda Mohamed akizungumza na wananchi kwenye ...