Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
leo tarehe 09 Januari, 2018 amekutana na kufanya mazungumzo na Waziri
Mkuu Mstaafu Mhe. Edward Ngoyai Lowassa, Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Baada ya mazungumzo hayo Mhe. Edward Ngoyai Lowassa amempongeza Mhe.
Rais Magufuli kwa kazi nzuri anayoifanya na ametaja baadhi ya maeneo
ambayo kazi kubwa imefanyika kuwa ni kutoa elimu bila malipo, ujenzi wa
mradi wa uzalishaji wa umeme katika maporomoko ya mto Rufiji (Stiegler’s
Gorge), ujenzi wa viwanda na ujenzi wa reli kwa kiwango cha kisasa
(Standard Gauge) ambavyo vinazalisha ajira nyingi kwa Watanzania.
“Nimepata faraja sana kuja hapa Ikulu kuonana na Mhe. Rais, tumezungumza
nae na nimempongeza kwa kazi nzuri anayoifanya, lazima tukiri anafanya
kazi nzuri na anahitaji kutiwa moyo.
“Moja kubwa ambalo ni la msingi sana ni la kujenga ajira, katika kuanza
ujenzi wa reli ya kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro hapo anajenga
ajira, na kwenye nchi yoyote inayoendelea suala muhimu ni kujenga ajira,
Stiegler;s Gorge ni kujenga ajira na mingine ya aina hiyo, lazima
kuwepo na kipaumbele cha kusema kwamba tunajenga ajira, jingine ni la
elimu, ni muhimu sana, hauwezi kuacha elimu katika mambo yako
unayofanya, hili nalo lazima lisemwe vya kutosha, kwa kweli nakushukuru
Mhe. Rais, you made my day” amesema Mhe. Lowassa.
Kwa upande wake Mhe. Rais Magufuli amempongeza Mhe. Edward Ngoyai
Lowassa kwa kutambua kazi kubwa inayofanywa na Serikali na amesema Mhe.
Lowassa ni mmoja wa viongozi ambaye kwa wakati wake ametoa mchango wake
katika nchi.
Mhe. Rais Magufuli ameongeza kuwa Mhe. Lowassa ni mwanasiasa mzuri kwani
hata wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu uliopita ambao naye aligombea
kiti cha Urais, hakuwahi kumtukana.
“Mhe. Lowassa ameniomba mara nyingi nikutane nae, na leo nimekutana nae,
tumezungumza mambo mengi, ameniambia ya kwake na mimi nimemwambia ya
kwangu, kwa ujumla Mhe. Lowassa ni mwanasiasa mzuri na tuendelee
kuwaenzi wazee hawa ambao kwa nyakati fulani walifanya mambo mazuri, na
mimi napenda kumpongeza Mhe. Lowassa ambaye kama alivyosema hapa kuwa
tumefanya mambo mazuri mengi.
“Ametaja miradi mbalimbali tunayotekeleza, ametaja mradi wa Stiegler’s
Gorge utakaogharimu zaidi ya Shilingi Trilioni 7, amezungumzia juu ya
elimu bure, amezungumzia juu ya maji ambayo kwa bahati nzuri yeye
alikuwa Waziri wa Maji na anafahamu sasa tumefikia wapi, amezungumza juu
ya umeme tulivyosambaza katika vijiji mbalimbali, elimu bure, huduma za
hospitali na mengine” amesema Mhe. Rais Magufuli.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
09 Januari, 2018
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Watumiaji wa Barabara Watakiwa Kutii Sheria za Usalama
Mkuu wa Kitengo cha Usalama barabarani Mkoa wa Kilimanjaro Mrakibu Msaidizi wa Polisi Sauda Mohamed akizungumza na wananchi kwenye ...
-
Na Omary Mlekwa HAI HALMASHAURI ya wilaya ya Hai, Mkoani Kilimanjaro, imetumia zaidi ya shilingi bil 13 ambayo ni sawa na asilimia ...
-
Meneja wa TARURA Wilaya ya Hai Mhandisi Charles Marwa (kulia) akitoa maelezo katika kijiji cha sanya station katika kata ya Kia ...
-
Inspector Shabo wa kituo cha polisi Bomang'ombe wakati akizungumza katika kikao cha mamlaka ya mji mdogo wa Hai Mwenyekiti...
No comments:
Post a Comment