Waziri Suleiman Jaffo akisalimiana na wakuu wa idara mbali mbali katika Halmashauri ya Wilaya ya Hai |
Na Adrian Lyapembile_HAI
WAZIRI wa
Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)Mhe.
Selemani Jaffo ameipongeza halmashauri ya wilaya ya hai kwa kuendelea kuboresha
miundombinu katika hospitali ya wilaya hiyo itakayofanikisha azma ya serikali
ya kutoa huduma bora za afya kwa wananchi wake.
Mhe. Jaffo
ameyasema hayo kwenye ziara yake ya kikazi katika wilaya ya Hai ambapo
ametembelea hospitali ya wilaya hiyo kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo
ikiwemo ujenzi wa wodi ya magonjwa mchanganyiko, ununuzi wa jenereta la kisasa
la kufua umeme pamoja na ujenzi wa duka la dawa.
Amesema
hatua iliyofikiwa ni nzuri kwenye ujenzi wa jengo la wagonjwa mchanganyiko na
duka la dawa huku akiongeza kuwa uwepo wa duka la dawa la kuaminika katika
wilaya ni jambo jema ambalo litasaidia wananchi wa wilaya ya Hai na maeneo
jirani kupata dawa kwa uhakika.
Mapema
akitoa maelezo ya ujenzi huo Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya
Hai Yohana Sintoo amemwambia waziri Jaffo kuwa ujenzi wa duka la dawa
umekamilika na kwamba kinachofanyika kwa sasa ni kuweka samani pamoja na
kufunga vifaa vinavyohitajika.
Naye Kaimu
Mganga Mkuu wa Wilaya Dk. Irene Haule amesema pamoja na kuwa jengo hilo
limejengwa maalumu kwa ajili ya wanachama wa bima za afya lakini litatumika
kama kitega uchumu kwa hospitali hiyo ambapo litatoa huduma kwa wagonjwa
wengine wasio wanachama wa bima ambao watanunua dawa lengo kuu likiwa ni
kuondoa tatizo la kukosekana dawa kwenye hospitali ya wilaya na maeneo ya
jirani.
No comments:
Post a Comment