Tuesday, 30 January 2018

Matokeo kidato cha nne yatangazwa : Shule 10 zilizofanya vizuri kitaifa hizi hapa

HABARI

Baraza la mitihani Tanzania (NECTA), limetangaza matokeo ya Kidato cha Nne na shule zilizofanya vizuri kwa mwaka 2017 ambapo Jumla ya watahiniwa 385,767 walisailiwa kufanya mtihani.

Akitangaza matokeo hayo leo mbele ya waandishi wa Habari, Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Mitihani Tanzania (NECTA), Dkt. Charles Msonde ametaja shule hizo kuwa kuwa ni St. Francis Girls, Feza Boys, Kemebos, Bethel Saabs Girls, Anuarite, Marian Gilrs, Canossa, Feza Girls, Marian Boys na Shamsiye Boys.

Hata hivyo, Dkt. Msonde ametaja shule 10 zilizofanya vibaya katika mtihani wa taifa ni : Kusini, Pwani Mchangani, Mwenge, Langoni, Furaha, Mbesa, Kabugaro, Chokocho, Nyeburu na Mtule.

No comments:

Watumiaji wa Barabara Watakiwa Kutii Sheria za Usalama

Mkuu wa Kitengo cha Usalama barabarani Mkoa wa Kilimanjaro Mrakibu Msaidizi wa Polisi Sauda Mohamed akizungumza na wananchi kwenye ...